Mwanzo

     

     

Kamusi Elezo ya Kiswahili

Karibu kwenye Wikipedia ya Kiswahili!

Wikipedia ni mradi wa kuandika kamusi elezo kamili na sahihi ya maandishi huru.

Kila mtu anaweza kuhariri makala yoyote, kutoa makosa ya lugha, kutohoa maneno na kuendeleza na kukuza makala, kwa kuandika kwa ufupi au kwa urefu. Tunakushauri ujiandikishe na kufungua akaunti. Angalia Wikipedia:Mwongozo ili ujifunze unavyoweza kuhariri au kusanifisha ukurasa. Usisite kushiriki; kwa sababu huu ni mradi wa ushirikiano, na hautaisha kamwe. Kamusi elezo itaimarika vizuri zaidi kila wakati. Angalia ukurasa wa jumuia, ukurasa wa jamii, na ule wa makala za msingi za kamusi elezo ili kung'amua unaweza kufanya kazi zipi ili kuboresha Wikipedia.


Je, wajua...

Kutoka kwenye mkusanyiko wa makala za Wikipedia:

Ngorongoro

  • ... kwamba Hifadhi ya Ngorongoro imepokewa katika orodha ya urithi wa dunia ya UNESCO?
  • ... kwamba Asha-Rose Mtengeti Migiro ni mwanasiasa wa kwanza kutoka nchini Tanzania aliyepata kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa?
  • ... kwamba Septemba 1752 ilikosa siku kumi na moja? Katika Dola la Uingereza, ulikuwa mwaka pekee wenye siku 355, kwani Septemba 3-13 zilirukwa wakati Dola lilipopitisha kalenda ya Gregori.
  • ... kwamba Samia Hassan Suluhu ni rais wa kwanza mwanamke Afrika ya Mashariki? Aliapishwa kuwa rais mara baada ya kifo cha mtangulizi wake, John Pombe Magufuli.


  • Makala ya wiki

    Papa Yohane Paulo II (kwa Kilatini: Ioannes Paulus PP. II; kwa Kiitalia: Giovanni Paolo II; kwa Kipolandi: Jan Paweł II; kwa Kiingereza: John Paul II; 18 Mei 1920 - 2 Aprili 2005) alikuwa Papa wa 264 kuanzia tarehe 16 Oktoba 1978 hadi kifo chake akidumu katika huduma hiyo kirefu kuliko Mapapa wengine wote, isipokuwa Mtume Petro na Papa Pius IX. Alitokea Wadowice, Krakow, Polandi.

    Alimfuata Papa Yohane Paulo I akiwa Papa wa kwanza asiye Mwitalia tangu miaka 455 iliyopita, wakati wa Mholanzi Papa Adrian VI (1522 - 1523), tena Papa wa kwanza kutoka Polandi (na makabila yoyote ya Waslavi) katika historia ya Kanisa. Alifuatwa na Papa Benedikto XVI.

    Jina lake la kuzaliwa lilikuwa Karol Józef Wojtyła (matamshi: ˈkarɔl ˈjuzɛf vɔiˈtɨwa).

    Wengi wanamhesabu kati ya watu walioathiri zaidi karne ya 20, hasa kwa sababu tangu mwanzo wa Upapa wake alipambana na Ukomunisti uliotesa nchi yake asili na nyinginezo, akachangia kwa kiasi kikubwa kikomo chake na kusambaratika kwa Urusi.

    Vilevile alilaumu ubepari wa nchi za magharibi na kudai haki katika jamii zote, akitetea hasa uhai wa binadamu na uhuru wa dini.

    Upande wa dini, aliboresha uhusiano kati ya Kanisa Katoliki na madhehebu mengine ya Ukristo[11] pamoja na ule na dini mbalimbali, kuanzia Uyahudi, Ubudha, Uislamu.

    Ziara zake 104 kati nchi 129 ulimwenguni kote, mbali na 146 nchini Italia na 317 katika parokia za Roma, zilikusanya mara nyingi umati mkubwa (hadi zaidi ya milioni 4 huko Manila, Ufilipino, mwishoni mwa siku ya kimataifa ya vijana), na kumfanya asafiri kuliko jumla ya mapapa wote waliomtangulia, akiwa mmojawapo kati ya viongozi wa dunia waliosafiri zaidi.

    Papa Wojtyła alitangaza wenye heri 1,340 na watakatifu 483, ili kuwapa Wakristo wa leo vielelezo mbalimbali kwa maisha yao ili walenge utakatifu walioitiwa na Mungu. Idadi hiyo ni kubwa kuliko ile ya waliotangazwa na jumla ya Mapapa wote waliomtangulia walau katika karne tano za mwisho.

    Alikuwa anaongea lugha mbalimbali, zikiwemo za Kipolandi, Kiitalia, Kifaransa, Kijerumani, Kiingereza, Kihispania, Kireno, Kiukraina, Kirusi, Kiserbokroatia, Kiesperanto, Kilatini na Kigiriki cha kale.

    Yohane Paulo II alitangazwa na mwandamizi wake Papa Benedikto XVI kuwa mwenye heri tarehe 1 Mei 2011, halafu Papa Fransisko akamtangaza mtakatifu tarehe 27 Aprili 2014.

    Sikukuu yake huadhimishwa kila mwaka tarehe 22 Oktoba[26], kulingana na siku ya kuanza rasmi huduma yake ya Kipapa kwa Misa iliyofanyika katika uwanja mbele ya Basilika la Mt. Petro, Vatikani. ►Soma zaidi


    Picha nzuri ya wiki

    Mlango wa Kiswahili wa Lamu

    Mlango Kiswahili wa Lamu ni moja ya vielelezo bora vya usanifu wa Kiswahili unaopatikana pwani ya Afrika Mashariki. Milango hii yenye urembo wa kuchongwa kwa ustadi mkubwa ni ishara ya utajiri wa historia na utamaduni wa Waswahili. Mbao zinazotumika mara nyingi ni za mti mgumu kama mninga au mkongo, huku nakshi zake zikionyesha mchanganyiko wa athari za Kiarabu, Kihindi, na Kiafrika. Mara nyingi, milango hii ilikuwa ishara ya hadhi ya kijamii na ilitumika kufikisha ujumbe kupitia michoro na maandishi ya Kiarabu. Leo hii, milango ya Kiswahili inahifadhiwa kama urithi wa kitamaduni na kivutio cha watalii katika miji ya kihistoria kama Lamu na Zanzibar.

    Takwimu ya Wikipedia ya Kiswahili

    • Idadi ya makala: 98,624
    • Idadi ya kurasa zote: 196,132 (pamoja na kurasa za watumiaji, majadiliano, msaada n.k.)
    • Idadi ya hariri: 1,408,893
    • Idadi ya watumiaji waliojiandikisha: 75,500
    • Idadi ya wakabidhi: 15
    • Idadi ya watumiaji hai: 629 (Watumiaji waliojiandikisha na kuchangia katika muda wa siku 30 zilizopita)
    Bofya hapa kwa kupata namba za sasa
    Katika mwezi wa Agosti 2020 wikipedia ya Kiswahili iliangaliwa mara milioni 1.73 hivi, ambayo ni sawa na mara 55,800 kwa siku au mara 2,326 kila saa. Asilimia 52 za wasomaji wetu wako Tanzania, asilimia 13 wako Kenya, asilimia 18 wako Marekani na mnamo asilimia 10 wako Ulaya.
    Angalia idadi ya wasomaji kwa makala mbalimbali
    (fungua anwani kwa browser yako, ondoa majina yaliyopo na ingiza jina la makala (hadi makala 10) unayopenda. Unaweza kubadilisha kipindi cha taarifa utakachoona; takwimu kabla ya 2015 hapa)
    • na makala 100 zilizotazamiwa zaidi "Topviews" kwa kipindi fulani.
    (unachagua kati ya makala 100 kwa mwezi au kwa siku)

    Michango ya wanawiki: angalia hapa michango ya mtumiaji kwenye kila mradi wa Wikimedia (andika jina la mtumiaji kwenye sanduku)

    Jumuia za Wikimedia

    Commons
    Ghala ya Nyaraka za Picha na Sauti
    Meta-Wiki
    Uratibu wa Miradi yote ya Wikimedia
    Wikamusi
    Kamusi na Tesauri
    Wikitabu
    Vitabu vya bure na Miongozo ya Kufundishia
    Wikidondoo
    Mkusanyiko wa Nukuu Huria
    Wikichanzo (Wikisource)
    Matini za vyanzo asilia kwa Kiswahili
    Wikispishi
    Kamusi ya Spishi
    Wikichuo
    Jumuia ya elimu
    Wikihabari
    Habari Huru na Bure


    Lugha

    Follow Lee on X/Twitter - Father, Husband, Serial builder creating AI, crypto, games & web tools. We are friends :) AI Will Come To Life!

    Check out: eBank.nz (Art Generator) | Netwrck.com (AI Tools) | Text-Generator.io (AI API) | BitBank.nz (Crypto AI) | ReadingTime (Kids Reading) | RewordGame | BigMultiplayerChess | WebFiddle | How.nz | Helix AI Assistant